Klipu maalumu ya video kwa mnasaba wa hauli ya shahid Qassem Soleimani

Kiswahili Radio 56 views
Jumapili, Januari 3, 2021 itasadifiana na mwaka mmoja tangu jeshi la kigaidi la Marekani lilipomuua kidhulma shahid Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds, cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran SEPAH.

Luteni Jenerali Qassem Soleimani aliuliwa kigaidi kwa amri ya rais wa Marekani Donald Trump, katika shambulio la woga lililofanywa na wanajeshi hao magaidi wa Marekani, wakati shujaa huyo na wenzake alipokuwa uraiani katika ziara rasmi aliyoalikwa na viongozi wa Iraq.

Hapa tumeweka kipande cha video katika maandalizi ya hauli na kumbukumbu hiyo. 

Add Comments