Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) linafanya mazoezi makubwa ya makombora katika jangwa la kati mwa Iran ambapo limefanyia majaribio makombora mapya ya balistiki na ndege za kivita zisizo na rubani au drone.
Awamu ya kwanza ya mazoezi hayo yaliyopewa jina la Mtume Mtukufu (SAW) ilianza jana Ijumaa ambapo makombora ya balistiki ya kizazi kipya yalivurumishwa mutawalia. Aidha ndege za kivita zisizo na rubani au drone zilitekeleza oparesheni kadhaa katika mazoezi hayo.
Mazoezo hayo yamehudhuriwa na Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Meja Jenerali Hossein Salami na Kamanda wa Kikosi cha Anga cha IRGC Jenerali Amir-Ali Hajizadeh.
Makombora ambayo yalifanyiwa majaribio katika mazoezi hayo ya Ijumaa ni pamoja na Zulfiqar, Zelzal, na Dezful