Kamanda wa ngazi za juu wa wavamizi wa Yemen aangamizwa kusini mwa Ma'rib

Kiswahili Radio 39 views
Vyombo mbalimbali vya habari vimeripoti kuwa, Meja Jenerali Nasser al Dhaibani, kamanda wa ngazi za juu zaidi wa muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia ameangamizwa katika mapigano ya kusini mwa mkoa wa Ma'rib nchini Yemen.

Vyombo hivyo vya habari likiwemo shirika la habari la Mehr na shirika la habari la al Khabar al Yamani pamoja na televisheni ya al Alam na nyinginezo zimenukuu maripota wao pamoja na taarifa ya chama cha Islah chenye mfungamano na serikali iliyojiuzulu ya Abdu Rabbuh Mansour Hadi na kutangaza kuwa, Meja Jenerali Nasser al Dhaibani ameangamizwa katika medani ya vita ya al Balaq, kusini mwa Ma'rib.

Televisheni ya al Alam imemuhoji ripota wake na kuthibitisha habari hiyo. Televisheni ya al Jazeera ya Qatar nayo imemnukuuu ripota wake akisema kuwa, kamanda huyo wa ngazi za juu kabisa wa muungano vamizi unaoongozwa na Saudia ameangamizwa katika mapigano makali baina ya mamluki wa wavamizi wa Yemen na jeshi la nchi hiyo linaloshirikiana na kamati za ukombozi za kujitolea za wananchi wa Yemen.

Add Comments