Maduro: Dunia inapaswa kulaani mauaji ya Jenerali Soleimani

Kiswahili Radio 105 views
Rais Nicholas Maduro wa Venezuela amesema jamii ya kimataifa inapaswa kulaani vikali mauaji ya kigaidi ya mwaka 2020 ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani wa Iran ambaye alikuwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya ugaidi.

Akizungumza katika mahojiano na televisheni ya Al Mayadeen ya Lebanon, Maduro amelaani mauaji ya Soleimani yaliyofanywa na Marekani na kuyataja kuwa ni jinai ya kuogofya.

Amesema Shahidi Soleimani alipambana na magaidi na watenda jinai ambao walikuwa wakiwashambulia raia wa kawaida na Mhimili wa Muqawama. "Alikuwa shujaa," amesema Maduro.

Add Comments