Iran Yazindua kituo kikubwa cha chini ya ardhi cha makombora Ghuba ya Uajemi + VIDEO

Kiswahili Radio 106 views
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limezindua kituo kikubwa na cha kistratijia cha makombora chini ya ardhi katika eneo la Ghuba ya Uajemi.

Sherehe za uzinduzi huo zimefanyika Ijumaa na kuhudhuriwa na Meja Jenerali Hussein Salami Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC). Akizungumza katika uzinduzi huo, Meja Jenerali Salami amesema mantiki ya IRGC ya kulinda mamlaka ya kujitawala, uhuru na mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu inazidi kupata nguvu.

Aidha amesema kituo hicho kikubwa cha makombora ya kistratijia cha chini ya ardhi ambacho kinamilikiwa na Kikosi cha Majini cha IRGC ni kati ya vituo kadhaa vya kistratijia vya IRGC vyenye maghala makubwa ya makombora.

Add Comments