Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) lalaani unyama wa Israel dhidi ya Wapalestina

Kiswahili Radio 66 views
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limelaani vitendo vya kinyama na uadui vinavyofanywa na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi wa taifa madhulumu la Palestina vikiwemo vya kuua raia wasio na hatia.

Kupitia tamko lililosomwa leo Alkhamisi na Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania Abubakar Zubeir bin Ally, Bakwata limeeleza kuwa vitendo hivyo vinavyofanywa na Israel vinakwenda kinyume na misingi ya haki za binadamu na vinapingana pia na misingi ya dini kuu duniani, ukiwemo Uislamu.

Tamko hilo la Baraza Kuu la Waislamu Tanzania limeitaka Jumuiya Kimataifa ichuke hatua zinazohitajika kusitisha udhalimu huo usiokubalika unaofanywa na utawala ghasibu wa Kizayuni.

Add Comments